VIONGOZI WA DINI NCHINI WAMETAKIWA KUWAELIMISHA WAUMINI WAO KUACHANA NA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO

VIONGOZI WA DINI NCHINI WAMETAKIWA KUWAELIMISHA WAUMINI WAO KUACHANA NA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO

Like
212
0
Wednesday, 04 February 2015
Local News

VIONGOZI wa dini nchini wametakiwa kuwaelimisha waumini wao kuachana na matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano ili kuinusuru jamii na athari mbaya za mitandao hiyo.

Akizungumza katika semina ya viongozi wa dini leo jijini Dar es salaam iliyo andaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini -TCRA- Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Profesa JOHN NKOMA amewataka viongozi wa dini kuwaelimisha waumini wao kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano kwani ina mchango mkubwa katika kuharibu maadili ya jamii hususani vijana na watoto.

Profesa Nkoma amevitaka vyombo vya habari vya Redio na Televisheni kuepuka vipindi vya mazungumzo yanayopaswa kufanyika usiku katika nyakati za mchana ili kusaidia kulinda maadili ya jamii yanayoharibika kwa kasi kubwa.

 

Comments are closed.