VIONGOZI WA MATAIFA WATUA NCHINI KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA MAGUFULI

VIONGOZI WA MATAIFA WATUA NCHINI KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA MAGUFULI

Like
299
0
Wednesday, 04 November 2015
Local News

VIONGOZI mbalimbali wameanza kuwasili nchini kwa ajili ya kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo kesho Novemba tano.

 

Miongoni mwa Viongozi wanaotarajiwa kushiriki sherehe hizo ni pamoja na marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Robert Mugabe wa Zimbabwe, Yoweri  Kaguta Museveni  wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Jacob Zuma  wa Afrika Kusini , Joseph Kabila  wa DRC, Filipe Nyusi  wa Msumbiji na  Edgar Lungu  wa Zambia.

 

Akiwa amevuta hisia za watu wengi hususani Waamini wa Dini ya Kikristu, Mhubiri maarufu  kutoka Nigeria TB Joshua atakuwa pia  ni miongoni mwa wageni mashuhuri watakaohudhuria sherehe hizo za kumuapisha Dokta John Pombe Magufuli kuwa rais mpya wa Tanzania awamu ya tano .

Comments are closed.