VIONGOZI WA NCHI 15 ZA SADC KUKUTANA LEO BOTSWANA

VIONGOZI WA NCHI 15 ZA SADC KUKUTANA LEO BOTSWANA

Like
248
0
Monday, 17 August 2015
Global News

VIONGOZI wa Mataifa 15 ya Jumuia ya Nchi za Kusini mwa Afrika- SADC, wanatarajia kukutana leo nchini Botswana katika Mkutano wao wa Mwaka.

Mkutano huo unafanyika wakati eneo hilo linakumbwa na upungufu wa chakula ambapo watu wanaokadiriwa kufikia milioni 27.4 kutoka idadi ya jumla ya wakazi 292, wa eneo hilo wanategemea msaada wa chakula ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Msemaji wa Shirika la Mpango wa chakula wa Dunia-WFO, David Orr, ameliambia shirika la habari la Ufaransa-AFP kuwa Zimbabwe na Malawi zinakabiliwa na tatizo la usalama wa chakula.

Comments are closed.