VIONGOZI WA NCHI ZA MAGHARIBI WAMEPENDEKEZA MIPANGO MIPYA JUU YA MGOGORO WA UKRAINE

VIONGOZI WA NCHI ZA MAGHARIBI WAMEPENDEKEZA MIPANGO MIPYA JUU YA MGOGORO WA UKRAINE

Like
250
0
Friday, 06 February 2015
Global News

WAKATI mapigano yakiendelea mashariki mwa Ukraine, viongozi wa nchi za magharibi wamependekeza mipango mipya kujaribu kumaliza mgogoro kati ya Majeshi ya Serikali na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesema mapendekezo mapya yaliyotolewa na kiongozi wa Ujerumani Kansela Angela Merkel, na rais wa Ufaransa Bwana Francois Hollande, yameongeza matumaini ya kumaliza mapigano.

Mpango huo utawasilishwa kwa Urusi Ijumaa, ambako Urusi imeahidi mazungumzo yenye manufaa. Lakini hatua ya Urusi kuwaunga mkono waasi wa Ukraine imeshutumiwa na Marekani.

 

Comments are closed.