VIONGOZI WA SIASA WAMETAKIWA KUHAMASISHA WAFUASI WAO KUTOVUNJA AMANI

VIONGOZI WA SIASA WAMETAKIWA KUHAMASISHA WAFUASI WAO KUTOVUNJA AMANI

Like
245
0
Tuesday, 13 October 2015
Local News

OFISI ya Msajili wa Vyama  Vya Siasa imewaasa na kuwataka viongozi wote wa  vyama  vya siasa kutoa kauli na maelekezo kwa wafuasi wao na wanachama wa vyama vyao kutoshiriki katika aina yoyote ile ya uvunjifu wa amani.

 

Hayo yamesemwa  na Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dares Salaam.

 

Jaji Mutungi amesema kuwa Dhamana ya nchi ipo mikononi mwa wananchi hivyo ushawishi wowote ule wa uvunjifu wa Amani unaweza kuliingiza Taifa katika machafuko yasiyo ya lazima.

Comments are closed.