VIONGOZI WA ULAYA WAUNGANA KUIKABILI URUSI

VIONGOZI WA ULAYA WAUNGANA KUIKABILI URUSI

Like
275
0
Friday, 19 December 2014
Global News

VIONGOZI wa Ulaya wamemaliza kikao chao mjini Brussels Ubelgiji, wakisema kwa sasa wameungana zaidi kuliko ilivyokuwa katika kuikabili Urusi.

Viongozi hao wameonyesha kuwa vikwazo vya kiuchumi havitadhoofishwa licha ya matatizo ya kifedha yanayoikabili Urusi.

Rais mpya wa Baraza la Ulaya, DONALD TUSK akifunga kikao cha viongozi wa EU amesema Urusi na vitendo vyake ni tatizo kubwa la kimkakati linaloikabili Ulaya.

 

Comments are closed.