VIONGOZI WA VIJIJI MANYARA WATAKIWA KUFANYA MAAMUZI KWA KUFUATA SHERIA KUMALIZA MIGOGORO

VIONGOZI WA VIJIJI MANYARA WATAKIWA KUFANYA MAAMUZI KWA KUFUATA SHERIA KUMALIZA MIGOGORO

Like
267
0
Friday, 07 August 2015
Local News

VIONGOZI wa vijiji katika Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wametakiwa kufanya maamuzi kwa kufuata sheria ili kumaliza migogoro ya ardhi kwa kutotoa nafasi kwa watu wanaotumia fedha kujipatia ardhi.

Mkuu wa wilaya hiyo Crispin Meela ameyasema hayo katika kijiji cha Kiongozi wakati akizungumza na wakazi wa eneo hilo kuhusiana na migogoro ya ardhi ambayo imekithiri vya kutosha wilayani humo.

Aidha amesema sheria inapaswa kusimamiwa kwani watendaji hao wanatambua wazi kuwa mtu mwenye fedha hana haki kwenye mgogoro lakini wanajipa upofu wa macho kutokana na maslahi ya watu wachache jambo ambalo halikubaliki.

Comments are closed.