VIONGOZI WAMETAKIWA KUTIMIZA AHADI ZAO KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

VIONGOZI WAMETAKIWA KUTIMIZA AHADI ZAO KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

Like
241
0
Tuesday, 01 December 2015
Global News

RAIS wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa ahadi zinazotolewa na viongozi zinahitaji kutekelezwa ili kuuokoa ulimwengu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hollande ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa viongozi wa dunia mjini Paris kwa lengo la kujadili juu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Katika mkutano huo Viongozi hao wameahidi kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ya mkaa inayosababisha viwango hivyo vya joto kuongezeka.

Comments are closed.