VIPODOZI HARAMU VYAKAMATWA BANDARI KUU MALINDI ZANZIBAR

VIPODOZI HARAMU VYAKAMATWA BANDARI KUU MALINDI ZANZIBAR

Like
388
0
Thursday, 26 November 2015
Local News
BODI ya Chakula, Dawa na Vipodozi imekamata vipodozi haramu katika Bandari Kuu ya Malindi Zanzibar ambavyo vimepigwa marufuku kuingizwa nchini.
 
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofini kwake Mombasa Mkaguzi wa Bodi hiyo Nassir Buheti amesema vipodozi hivyo haramu vimepigwa marufuku kuingizwa nchini kutokana na kuwa na Viambata vyenye kemikali vinavyoweza kuleta madhara kwa Mtumiaji ikiwemo Kansa.
 
Amevitaja vipodozi hivyo kuwa ni pamoja na Movet Crèame kutoka Itali na Medical Fade Crème kutoka Marekani vyenye uzito wa tani tatu vilivyokuwa vimehifadhiwa katika Makontena yaliyochanganywa na vitu vingine bandarini hapo.
ZANZZ
Baadhi ya vipodozi vilivyokamatwa

Comments are closed.