VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NI JUKUMU LA KILA MMOJA WETU

VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NI JUKUMU LA KILA MMOJA WETU

Like
278
0
Wednesday, 04 May 2016
Local News

JAMII imetakiwa kushirikiana na Serikali pamoja na Sekta binafsi zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya kwani vita hiyo ni ya kila Mtanzania mwenye nia njema na vijana.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kusaidia waathirika wa Dawa za kulevya cha Pili Misana Foundation kilichopo Kigamboni jijini Dar es salaam Bi Pili Misana alipozungumza na Waandishi wa habari katika hafla ya kituo hicho kufikisha miaka minne tangu kuanzishwa kwake.

Bi. Misana amesema tangu kuanzishwa kwa vituo hivyo mwaka 2013 hadi sasa kimesaidia zaidi ya Waathirika wa dawa za kulevya Elfu Mbili ambao tayari wamerejea katika shughuli zao mbali mbali za kujenga Taifa.

Comments are closed.