WANAWAKE nchini wametakiwa kuachana na matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango na badala yake watumie njia asilia ili kuepuka madhara yatokanayo na njia za kisasa.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la kutetea uhai Pro-life wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na masuala ya afya ya uzazi na uzazi salama kwa akina mama.
Amesema kuwa shirika hilo limeweka mikakati ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo za utoaji mimba, elimu ya ngono pamoja na matumizi ya njia za uzazi wa mpango.