VITUO VYA AFYA VYAZOROTA MWANZA KUFUATIA KUKOSEKANA KWA UMEME

VITUO VYA AFYA VYAZOROTA MWANZA KUFUATIA KUKOSEKANA KWA UMEME

Like
293
0
Tuesday, 25 August 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa kukosekana kwa huduma ya umeme  katika baadhi ya vituo vya afya Jijini Mwanza kumesababisha kuzorota kwa upatikanaji wa huduma katika vituo hivyo.

Zainabu Chambo ni Muuguzi kutoka zahanati ya Buhongwa iliyopo wilaya ya Nyamagana Jijini humo amesema hali hiyo husababisha mama wajamzito kwenda kutafuta zahanati nyingine kwa umbali mrefu  kwaajili ya kupatiwa huduma hali inayowalazimu kutoa kiasi kikubwa cha fedha.

Zainabu amesema  kitendo cha kukosekana kwa umeme kimewawia vigumu wao kufanya ufuatiliaji na kujua nani ana matatizo na wanaoathirika zaidi ni wakinamama ambao wanaujauzito wa kwanza.

Comments are closed.