IMEELEZWA kuwa viwango vya Mimba za Utotoni Vimepungua na Upatikanaji wa Huduma za Afya ya Uzazi kwa Vijana imeongezeka kufatia mpango wa Uelimishaji unaofanywa na Shirika la Afya na Utafiti Afrika- AMREF
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dokta Flavian Gowele alipokuwa Mgeni rasmi katika Uwasilishaji wa Ripoti ya Utafiti uliofanywa na shirika hilo kwa kipindi cha miaka minne katika Wilaya za Ilala, Kinondoni na Iringa ambapo Takwimu zinaonyesha kuwa viwango vya Mimba za Utotoni zimeshuka kutoka asilimia nane miaka minne iliyopita hadi asilimia mbili.