VOLKENO: VIWANJA VYA NDEGE VYAFUNGWA INDONESIA

VOLKENO: VIWANJA VYA NDEGE VYAFUNGWA INDONESIA

Like
334
0
Friday, 17 July 2015
Global News

MIRIPUKO miwili ya Volkeno iliyotokea jana imesababisha viwanja vya ndege vitatu kufungwa nchini Indonesia, kikiwamo kiwanja cha ndege cha mji mkuu wa pili Surabaya.

Mlima wa Raung ulioko katika kisiwa kikuu cha Java umetoa uchafu wa majivu wa hadi mita 2,000 hewani baada ya miungurumo ya wiki kadhaa na mlima wa Gamalama mashariki mwa Indonesia uliripuka pia hapo jana baada ya miezi kadhaa ya tulivu.

Miripuko hiyo imejiri katika nchi hiyo yenye idadi kubwa kabisa ya waislamu wakati ambao mamilioni ya watu wanasafiri nchini kuelekea mijini kwao kwa kusheherekea sikukuu ya Iddi baada ya mfungo wa mwezi wa Ramadhan.

FD2

Picha ni uwanja wa ndege wa Juanda

Comments are closed.