VOLKSWAGEN YATANGAZA KUNUNUA MAGARI YAKE

VOLKSWAGEN YATANGAZA KUNUNUA MAGARI YAKE

Like
256
0
Friday, 22 April 2016
Global News

KAMPUNI ya magari ya Volkswagen imetangaza kuyanunua magari ya kampuni yake kutoka kwa wateja nchini Marekani yapatayo laki tano kama sehemu ya kutimiza makubaliano yaliyoafikiwa na idara ya sheria ya Marekani dhidi ya kampuni hiyo kuhusika na kashfa ya uchafuzi wa hali ya hewa.

Jaji kutoka San Francisco hajabainisha wazi kiasi ambacho wamiliki wa magari hayo watalipwa na kampuni ya Volkswagen pale watakapo iuzia kampuni hiyo magari yake wanayoyamiliki.

Makubaliano mengine yaliyofikiwa ni kwamba Volkswagen itatakiwa kutoa fungu la fedha ili kuhamasisha tekinolojia ya kijani ya kukabiliana na uchafuzi wa hali ya hewa.

Comments are closed.