VPL: YANGA, SIMBA NA AZAM MWENDO WA KUGAWA DOZI

VPL: YANGA, SIMBA NA AZAM MWENDO WA KUGAWA DOZI

Like
388
0
Thursday, 01 October 2015
Slider

Miamba ya soka Tanzania Yanga, Simba pamoja na Azam FC wameendelea kung’aa katika michezo ya ligi kuu iliyotimua vumbi hapo jana.

Katika jiji la Morogoro Mtibwa Sugar iliikaribisha Yanga huku mchezo huo ukimalizika kwa wenyeji hao wakilazimika kupokea kichapo cha magoli 2-0 magoli yaliyotiwa nyavuni na Malimi Busungu na Donald Ngoma matokeo yanayoifanya klabu hii kongwe kuwa kileleni na kuongoza ligi kwa alama 15.

Azam nao wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Azam Complex wameiadhibu klabu ya Coastal Union ya Tanga, mabao 2-0 yaliyotiwa nyavuni na Shomari Kapombe na Kipre Tche Tche.

Wekundu wa Msimbazi Simba wakawachapa Stand United kwa bao 1-0 bao hilo pekee likiwekwa kimiani na Joseph Kimwaga.

Matokeo mengine ya michezo ya ligi hiyo

African Sports 0-1 Mgambo

Kagera Sugar 0-0 JKT Ruvu

Majimaji FC 1-1 Ndanda FC

Prisons 0-0 Mwadui FC 0

Comments are closed.