VURUGU ZAPELEKEA KUVUNJIKA KWA MKUTANO WA MADIWANI KINONDONI

VURUGU ZAPELEKEA KUVUNJIKA KWA MKUTANO WA MADIWANI KINONDONI

Like
379
0
Friday, 11 December 2015
Local News

MKUTANO wa baraza la Madiwani wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam umelazimika kuvunjika kufatia vurugu zilizojitokeza kutokana na baadhi ya wabunge na Mdiwani wa Zanzibar wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi-CCM- kuingia katika kikao hicho jambo ambalo vyama vya UKAWA vimepinga.

 

Mkurugenzi wa Manispaa ya hiyo Mussa Natti amesema ameahirisha kikao hicho hadi hapo ufafanuzi wa kisheria juu ya Wabunge hao utakapopatikana.

 

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibamba John Mnyika amesema kitendo hicho cha kuletwa kwa Wabunge  kutoka Zanzibar ni mbinu za chama tawala ili wapete ushindi katika uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es salaam.

Comments are closed.