VYAMA 21 VYA SIASA VIMESAINI MAADILI YA UCHAGUZI MKUU 2015

VYAMA 21 VYA SIASA VIMESAINI MAADILI YA UCHAGUZI MKUU 2015

Like
199
0
Tuesday, 28 July 2015
Local News

VYAMA vya Siasa 21 vinavyotarajiwa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu vimesaini Maadili ya uchaguzi yatakayotumika wakati wa kampeni, kupiga kura na wakati wa kutangaza matokeo.

Maadili hayo yanayohusisha Serikali,Tume ya Taifa ya Uchaguzi –NEC- na Vyama vya Siasa yalisainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu dokta Florence Turuka, Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva na Wawakilishi wa vyama vya Siasa 21 nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume hiyo amesema Chama cha Wananchi –CUF-hakikusaini Maadili hayo kutokana na kuwa na kazi nyingine lakini akasisitiza kuwa Chama hicho kitasaini wakati wowote.

Comments are closed.