VYAMA VYA SIASA VIMESHAURIWA KUZUNGUMZA NA WAFUASI WAO KUTII SHERIA

VYAMA VYA SIASA VIMESHAURIWA KUZUNGUMZA NA WAFUASI WAO KUTII SHERIA

Like
317
0
Thursday, 15 October 2015
Local News

BARAZA la Vyama vya Siasa nchini limevishauri vyama vya siasa kuzungumza na kuwasihi wafuasi wao kutii sheria bila shuruti ili kuendeleza amani iliyopo nchini.

 

Aidha Baraza hilo limeviomba Vyama kuwaeleza wafuasi na wapenzi wao kurudi majumbani na kuendelea na shughuli zao mara baada ya kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa hatua za uandikishwaji.

 

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Kikako maalumu cha Baraza hilo kilichofanyika mjini Zanzibar.

DSC_0212

baadhi ya waandishi walihudhuria mkutano huo

Comments are closed.