VYAMA VYA SIASA VIMETAKIWA KUWA MAKINI KATIKA KUSIMAMISHA WAGOMBEA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

VYAMA VYA SIASA VIMETAKIWA KUWA MAKINI KATIKA KUSIMAMISHA WAGOMBEA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Like
257
0
Friday, 31 July 2015
Local News

VYAMA vya siasa vya upinzani nchini vimetakiwa kuwa makini katika kusimamisha wagombea  hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu  ili kuepukana na wagombea wanaotumia  fedha katika kupata madaraka.

 

Kauli hiyo imetolewa  Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama cha Alliance for  Democratic change – ADC- Saidi Miraji alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya siasa nchini ambapo ameviasa vyama kusimamia msimamo yake.

 

Amewashauri kuwaweka wagombea ambao wanafahamu kwa undani na kuzingatia  misingi ya itikadi za vyama vyao, wenye msimamo na maadili katika kuleta Demokrasia ya kweli katika maendeleo ya nchi na sio  viongozi wanaofanya siasa kwa matakwa yao binafsi.

Comments are closed.