VYAMA VYA USHIRIKA VYAOMBA KUPEWA ELIMU YA SHERIA YA USHIRIKA

VYAMA VYA USHIRIKA VYAOMBA KUPEWA ELIMU YA SHERIA YA USHIRIKA

Like
339
0
Monday, 03 November 2014
Slider

VIONGOZI wa vyama  vya ushirika wilaya  ya Nachingwea mkoani Lindi wameiomba wizara ya kilimo na ushirika  kutoa elimu kwa wanachama  juu ya  sheria  mpya ya ushirika  ili iweze kutambulika na upunguza migogoro na mivutano inayosababisha vyama kugawanyika  na kukosa nguvu ya kiuchumi na uzalishaji.

Ombi hilo limetolewa  na viongozi wa vyama vya ushirika vya MAKINI , MKOTOKUYANA,NDOMONI na MARAMBO wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari wilayani humo.

MOHAMEDI MUSA mwenyekiti wa chama cha msingi Makini amesema  pamoja  na serikali  kuleta sheria mpya ya ushirika  lakini viongozi na wanachama  wa vyama hivyo  hawajaziona sheria  na serikali haina budi kutoa elimu kwa wanaushirika ili waweze kuzitambua.

Amesema kuwa  kuwepo kwa sheria hizo mpya kumevifanya vyama vya ushirika  kugawanyika na kusababisha  mapato ya vyama kuwa madogo jambo ambalo linatishia uhai  na kuwa nauwezekano wa kufa kwa vyama hivyo kutokana na kuwa na uzalishaji mdogo.

 

Comments are closed.