VYETI VYA KUZALIWA KUTUMIKA KUTOA VITAMBULISHO VYA TAIFA

VYETI VYA KUZALIWA KUTUMIKA KUTOA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Like
302
0
Monday, 10 November 2014
Local News

WATANZANIA wametakiwa kuwa na vyeti vya kuzaliwa ili waweze kuwa na sifa za kupewa vitambulisho vya Taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usajili, Ufilisi,na udhamini nchini-RITA PHILIP SALIBOKO ameeleza hayo alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari mjini Moshi Kilimanjaro.

Amebainisha kuwa ni vyema Watanzania wakawa na vyeti vya kuzaliwa kwani ni muhimu na vina mifumo inayotakiwa.

Aidha amewataka wananchi wa mkoa huo kushiriki katika mpango ulioanzishwa na RITA wa kugawa vyeti vya kuzaliwa mashuleni.

Comments are closed.