VYOMBO VYA HABARI NCHINI VIMETAKIWA KUACHA MZAHA KUEPUSHA MACHAFUKO KAMA YA BURUNDI

VYOMBO VYA HABARI NCHINI VIMETAKIWA KUACHA MZAHA KUEPUSHA MACHAFUKO KAMA YA BURUNDI

Like
248
0
Monday, 18 May 2015
Local News

VYOMBO vya Habari nchini vimetakiwa kuacha mzaha na kufanya kazi zake kisawasawa na kuboresha Demokrasia ili nchi isiingie katika machafuko kama yaliyotokea Burundi hivi karibuni.

Imeelezwa kuwa Vyombo vya Habari vinao wajibu mkubwa wa kusimamia Demokrasia na kuhakikisha hali za Binadamu zinazingatiwa ili viweze kutekeleza majukumu yake.

Hayo yamebainishwa na Mhadhiri wa Shule ya Uandishi wa Habari ya Chuo Kikuu cha Dar es salaa,Dokta AYOUB RIOBA,baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Saba wa wamiliki wa Vyombo vya Habari wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC.

Comments are closed.