VYOMBO VYA HABARI VIMEPONGEZWA KWA KUTOA HABARI ZA KUZUIA UHALIFU  KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

VYOMBO VYA HABARI VIMEPONGEZWA KWA KUTOA HABARI ZA KUZUIA UHALIFU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Like
181
0
Thursday, 22 October 2015
Local News

MKUU wa jeshi la polisi Nchini ERNEST MANGU amevipongeza vyombo vya habari nchini kwa kazi kubwa wanayofanya kuelimisha jamii hususani katika habari zinazosaidia kuzuia uhalifu na kuhamasisha wananchi kudumisha amani kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.

IGP Mangu amewaambia wandishi wa habari kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea kumalizika kwa kampeni za uchaguzi mkuu hali ya nchi kwa ujumla imeendelea kuwa shwari na jeshi la polisi limeweza kudhibiti kwa kukemea na kuwafikisha mahakani watu wachache waliofanya vitendo vyenye uvunjifu wa amani.

Comments are closed.