VYOMBO VYA HABARI VIMETAKIWA KUANDAA VIPINDI VYA KUELIMISHA JAMII

VYOMBO VYA HABARI VIMETAKIWA KUANDAA VIPINDI VYA KUELIMISHA JAMII

Like
407
0
Friday, 08 April 2016
Local News

VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuandaa vipindi vya kuelimisha na kupunguza burudani kwa kuongeza idadi ya vipindi vya kujenga uzalendo, amani, mshikamano pamoja na umoja wa kitaifa.

 

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Ziwa Enjinia. Lawi Odieri wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia Mkoani Simiyu.

 

Naye mheshimiwa Nauye amesema kuwa uwepo wa vituo vya kutosha vya utangazaji katika mkoa wa Simiyu vitasaidia kutangaza vivutio vya utalii wa kiutamaduni vilivyopo mkoani humo pamoja na kuinua wasanii wa mkoa huo kwa kuwapatia nafasi ya kurusha nyimbo zao katika vituo hivo.

Comments are closed.