VYOMBO VYA HABARI VIMETAKIWA KUTOA NAFASI SAWA KWA WAGOMBEA WOTE

VYOMBO VYA HABARI VIMETAKIWA KUTOA NAFASI SAWA KWA WAGOMBEA WOTE

Like
246
0
Friday, 18 September 2015
Local News

VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuwapa nafasi wagombea wote wa vyama vya kisiasa wanaoshiriki kujinadi kwenye kampeni ili watangaze sera zao kwa wananchi, kuliko kuvipa kipaumbele vyama viwili pekee vya CCM na Chadema.

 

Akizungumza jijini Arusha wakati wa warsha ya kuandika habari za uchaguzi kwa waandishi habari wa mikoa ya kanda ya kaskazini, mhariri mwandamizi nchini Chrysostom Rweyemamu amesema ni muda muafaka sasa kwa vyombo hivyo kuzingatia ipasavyo maadili yao kwa kutoa haki sawa kwa kila mmoja.

Comments are closed.