VYUO NA TAASISI ZA ELIMU ZIMETAKIWA KUTOA MAFUNZO YANAYOENDANA NA SOKO LA AJIRA

VYUO NA TAASISI ZA ELIMU ZIMETAKIWA KUTOA MAFUNZO YANAYOENDANA NA SOKO LA AJIRA

Like
253
0
Monday, 21 December 2015
Local News

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amevitaka vyuo na taasisi za elimu nchini kuhakikisha vinatoa mafunzo bora yanayoendana na mahitaji ya soko la ajira.

 

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika mahafali ya kwanza ya Shahada ya Takwimu Rasmi katika Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Balozi Sefue amesema ni vyema vyuo na taasisi za elimu zikahakikisha zinafanya tafiti ili kujua mahitaji ya wataalamu wanaotakiwa.

 

Hata hivyo serikali imekuwa mstari wa mbele kupitia Wizara ya Fedha kuhakikisha inakisaidia chuo hicho kukabiliana na changamoto zinazokikabili ikiwemo uhaba wa fedha za kuendeshea chuo hicho.

 

Comments are closed.