Waafrika wenye rangi nyeusi huwa na wakati mgumu pale wanapohitaji tiba ya dawa

Waafrika wenye rangi nyeusi huwa na wakati mgumu pale wanapohitaji tiba ya dawa

1
839
0
Tuesday, 12 November 2019
Global News

Waafrika wenye rangi nyeusi huwa na wakati mgumu pale wanapohitaji tiba ya dawa kwa sababu wanawakilisha asilimia mbili tu ya sampuli ya vina saba iliyotumika na utafiti wa kutengeneza dawa, lakini kampuni mpya ya Nigeria inataka kubadili mumo huo.

Uhaba wa tafiti kuhusu watu wa aina fulani unahatarisha kuenea kwa magonjwa duniani kote.

Kwa mujibu wa muasisi na mkurugenzi wa kampuni inayoangazia biolojia ya vina saba ‘ 54gene’ , Dkt. Ene-Obong, watu wenye rangi nyeusi wako na utofauti wa kimaumbile ofauti na watu wengine duniani , na kutengeneza taarifa zao za vina saba kuna uhitaji wa raslimali kubwa zaidi kupatikana.

Amefanya utafiti wa vinasaba katika maabara ya nchini Nigeria katika mji wa Lagos , ambapo timu yake ina mpango wa kufanyia utafiti vinasaba 4000 vya sampuli zitakazokusanywa kwa mwaka 2019, kwa malengo ya kuwafikia watu laki moja ifikapo miezi 12 ijayo.

Abasi Ene-Obong ameiongoza timu ya utafiti wa dawa ambazo zinaweza kutumika duniani kote

Dkt. Ene-Obong anasema kuwa ufahamu wa jukumu la vina saba katika magonjwa litasaidia katika uhusiano wa tiba .

“Dawa hazitengenezwi hata kwa kuwafikiria kuwa kuna waafrika wapo, idadi ya waafrika haifanyiwi majaribio ya kitabibu kulingana na mahitaji yao , kile kilichopo ni dawa ambazo hazina uwezo wa kutibu kiufanisi ,” alisema.

Dawa mpya pia inachukua muda mrefu kufika Afrika – mara nyingine ni kati ya miaka 15 mpaka 20 , alisema Dkt. Ene-Obong.

Watengenezaji wakubwa wa dawa huwa wanaangalia soko la mataifa ya magharibi, na aina ya vina saba vinavyopatikana barani Afrika baada ya makampuni hayo kupoteza wagonjwa wao.

Dkt Ene-Obong anasema kwamba anadhamiria kutatua tatizo hili kwa kuongeza upatikanaji wa takwimu za vina saba kutoka Afrika ili kuhamasisha utafiti wa kisayansi kufanyika zaidi kwa kuwaangazia watu hao.

“Mpango huo utatoa mwanya wa upatikanaji wa matokea ambayo yatawafanya waafrika wapate tiba kulingana nao lakini pia tiba ya kila mmoja ipatikane,” alisema.

Kampuni yake ina mpango wa kufanyia utafiti magonjwa kama ya selimundu(sickle cell), ugonjwa ambao unawaathiri waafrika zaidi.

Licha ya kuwa Dkt. Ene-Obong anasema kuwa ’54gene’ itaweza kubainisha namna ambavyo jenetiki inafanya kazi katika magonjwa ya muda mrefu na yasioambukiza kama saratani ,shinikizo la damu, ugonjwa wa kupoteza kumbukukumbu na mengineyo.

Kwa sasa wameanza katika hospitali za Nigeria ili kukusanya sampuli za DNA.

“Hatutaingilia huduma ambayo wagonjwa wanapata, lakini kwa ruhusa yao tutawaomba kupata damu au tishu za mwilini kwa ajili ya utafiti, alisema Dkt. Ene-Obong .

Vilevile amesema kampuni haina nia ya kuhifadhi tu lakini kuboresha huduma ya afya katika jamii inazozifanyia kazi.

Kampuni hiyo ilipokea ufadhili wa dola milioni 4.5 kutoka kwa wafadhili wakati ilipozindua mradi huo mwezi januari.

Fedha nyingi zilitumika kuongeza maabara zilizopo mjini Lagos, kukodisha wafanyakazi na kutengeneza mfumo wa kusambaza umeme kwa sababu Nigeria inakabiliwa na tatizo kubwa la kukatika umeme.

Presentational white space

Dkt. Ene-Obong aliacha kazi yake ya ushauri wa viongozi wa sekta ya dawa na kuanzisha kampuni yake ya 54gene, ambayo sasa imeweza kutengeza watafiti zaidi ya 30 ambao wamefanya kazi katika taasisi za tiba nchini Marekani na Uingereza.

Lengo letu ni kuhakikisha kuwa watu wanatibiwa kiwango kisichokua na utofauti na Marekani au Uingereza.

Jina la kampuni hiyo imetokana na majina ya nchi 54 za Afrika .

“Hatutakikuwa kampuni ya wanaijeria peke yake bali tuko na mazungumzo na nchi za Afrika mashariki, magharibi na kusini mwa Afrika”.

Ingawa alikuwa na hofu kuhusu miongozo iliyopo katika baadhi ya mataifa ya Afrika na kutokuepo na utayari.

“Tunafuatilia sheria muhimu za kuzifuata katika nchi husika ,kwa sababu baadhi ya nchi miongozo haiko wazi.Hivyo lazima kujiandaa kufuata sheria husika na kufuata utaratibu wa taifa husika.”

Kampuni hiyo itatunza taarifa iliyozipata kwa kufuata utaratibu.

Kuna baadhi ya serikali za Afrika kama Kenya na Uganda,mamlaka imependekeza kuwa wakusanye taarifa za vina saba ambazo zitasaidia kupambana na uhalifu

Lakini Dk Ene anasema kuwa kampuni yake haina nia ya kuzigawa taarifa wanazozitafuta ingawa kampuni hiyo iko radhi kutoa picha kubwa ya takwimu ili serikali kuweza kuelewa hali ya afya ya watu.

 

 

 

cc;BBCswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *