WAANGALIZI WA UCHAGUZI EAC WATOA RIPOTI YA AWALI

WAANGALIZI WA UCHAGUZI EAC WATOA RIPOTI YA AWALI

Like
220
0
Tuesday, 27 October 2015
Local News

WAANGALIZI wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC leo wametoa ripoti ya awali kuhusu Zoezi la uchaguzi linavyoendelea tangu kuanza kwa zoezi hilo la uchaguzi  na kusema kuwa zoezi hilo limemalizika vizuri katika maeneo mengi ya nchi.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam Kiongozi wa Timu ya Waangalizi kutoka EAC Mheshimiwa Arthur Moody Awori amesema kuwa kwa mara ya kwanza uchaguzi wa mwaka huu umekuwa wa ushindani mkubwa uliobebwa na mabishano bila ya kuwepo na vurugu zozote.

Aidha amebainisha kuwa kumekuwa na changamoto kwa wafanyakazi wa Nec kutopatiwa maslahi yao kwa wakati hivyo kuna haja ya kuboresha utendaji wa NEC ili chaguzi zijazo ziende vizuri.

Comments are closed.