WAASI SYRIA WATUMIA MATEKA KAMA NGAO

WAASI SYRIA WATUMIA MATEKA KAMA NGAO

Like
209
0
Monday, 02 November 2015
Global News

TAARIFA kutoka nchini Syria zinaeleza kwamba ,waasi nchini humo wanatumia askari mateka wanajeshi na wengine wenye uhusiano na serikali kama ngao yao ili kujikinga na mashambulizi ya askari wa serikali ya rais Bashar al-Assad.

Mkanda wa video uliooneshwa katika mitandao ya kijamii inaonesha wanawake na wanaume waliofungwa katika vikinga vya chuma vilivyowekwa nyuma ya malori na magari hayo kuendeshwa taratibu katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo Damascus.

Inasemekana video hiyo imetoka katika eneo linalokaliwa na waasi katika vitongoji vya mji wa Damascus,mahali palipotokea mashambulizi ya roketi ambalo liliua watu sabini katika eneo la soko mwishoni mwa juma lililopita.

Comments are closed.