WABUNGE wa Viti maalum Nchini wametakiwa kuelekeza Nguvu katika kugombea nafasi za ubunge Majimboni kama ilivyo kwa wanaume badala ya kuendelea kutegemea kupata nafasi hiyo kwa kuteuliwa.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoani Singida CHRISTOWAJA MTINDA wakati akizungumza na EFM ambapo amesema wakati wa Wanawake kusubiri kuteuliwa umepitwa na wakati hivyo ni vyema kufanya jitihada za kutosha kuwatumikia wananchi.
MTINDA amesema Umefika wakati ambapo wanawake wanapaswa kuonyesha kwa vitendo kuwa wanaweza kupitia kugombea nafasi mbali mbali za uongozi ikiwemo Udiwani Ubunge na hata nafasi ya Urais kwani tofauti ya jinsia isitumike kama ni kigezo kwa Mwanamke kusubiri nafasi ya kuteuliwa.