WABUNGE WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KUHAMASISHA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI WA VITUO VYA POLISI

WABUNGE WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KUHAMASISHA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI WA VITUO VYA POLISI

Like
196
0
Wednesday, 20 May 2015
Local News

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya nchi imewataka wabunge kushirikiana vyema na wizara hiyo katika kuhakikisha wanatoa hamasa kwa wananchi ili wapate mwamko wa kuchangia ujenzi wa vituo vya polisi katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha usalama.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu waziri wa wizara hiyo mheshimiwa PEREIRA SILIMA wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu jimbo la Mbeya dokta MARY MWANJELWA aliyetaka kufahamu jitihada za ujenzi wa kituo cha polisi cha Ilembo mkoani humo.

Mheshimiwa PEREIRA amesema kuwa endapo wananchi watapewa hamasa na elimu ya kutosha juu ya uchangiaji katika ujenzi wa vituo hivyo itarahisisha na kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta usalama  wa kutosha kwao na mali zao.

Comments are closed.