WADAU WA MAENDELEO WAMEOMBWA KUISAIDIA TAASISI YA TEEN GIRLS SUPPORTIVE

WADAU WA MAENDELEO WAMEOMBWA KUISAIDIA TAASISI YA TEEN GIRLS SUPPORTIVE

Like
296
0
Monday, 10 November 2014
Local News

WADAU mbalimbali wa Maendeleo wameombwa kushiriki ipasavyo katika kuisaidia Taasisi isiyo ya kiserikali ya TEEN GIRLS SUPPORTIVE ili kufanikisha lengo la kuwapatia Wasichana maarifa katika masuala ya Afya na Uchumi.

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na MARIAM JOSHUA ambaye ni mmoja wa Wanataasisi hiyo wakati wakifanya kampeni katika shule ya Sekondari ya King’ong’o juu ya Afya ya Uzazi na Maamuzi ya Kuchagua Kazi ya Kusomea.

MARIAM amebainisha kuwa kampeni hiyo ni endelevu na wanatarajia kuyafikia maeneo yote ya nchi ili kuwasaidia wasichana wengi waliopo mashuleni kuwa na uelewa juu ya masuala hayo.

Comments are closed.