Wafanyabiashara mbali mbali wenye maduka eneo la kariakoo wamefanya mgomo usio rasmi wa kufunga maduka yao ili kutokaguliwa na watendaji wa TRA ambao wanaendesha msako wa kuwakamata wale wote ambao wanatumia mashine za EFD kinyume na matumizi yake halisi.
Kwa mujibu wa hali halisi ambayo imeonekana leo katika eneo hilo maduka mengi yamefungwa katika kile kinachoonekana kukwepa kufanyiwa tathmini ya matumizi ya mashine za ki Electroniki za EFD zinazofanya kazi ya kutoa risiti na kutunza kumbukumbu za mahesabu za mwenye duka.
Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi ambaye aliongea na ripota wa EFM Bwana Sosthenes Shayo alisema wao hawapingi matumizi au kutumia mashine za EFD wanapinga mfumo mbaya uliowekwa kwa ajili ya matumizi ya mashine hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu Mamalaka ya Mapato -TRA -amesema kuwa kufuatia Uhakiki huo yapo mambo kadha wa kadha ambayo wameyabaini kufuatia zoezi hilo ikiwemo uhafifu wa matumizi ya mashine hizo.
Wafanyabiashara mara nyingi wanalalamika lakini tukiitisha vikao hawafiki. Na pia baadhi yao kwa maana ya wachache wenye hitilafu ndio wanachochea wengine kugoma ili waendelee na kutotumia mashine hizo. Efm itakuletea habari zaidi juu ya sakata hilo.