WAFANYABIASHARA SOKO LA BUGURUNI WAIOMBA MANISPAA YA ILALA KUWAJENGEA MIUNDOMBINU

WAFANYABIASHARA SOKO LA BUGURUNI WAIOMBA MANISPAA YA ILALA KUWAJENGEA MIUNDOMBINU

Like
400
0
Thursday, 06 November 2014
Local News

WAFANYABIASHARA wa Soko la Buguruni wameiomba Serikali kupitia manispaa ya Ilala kuwasaidia kuwajengea miundombinu ya soko hilo ili kuwasaidia kupunguza hasara ya uharibifu wa biashara zao.

Wakizungumza na kituo hiki  leo katika soko hilo wafanyabiashara  hao wamesema kuwa wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali za miundombinu hali inayosababisha kuharibika na kuoza kwa biashara zao hususani katika kipindi cha mvua.

Kituo hiki kilizungumza na Mwenyekiti wa soko hilo Said Habibu ambaye amekiri kuwepo kwa changamoto hizo na kudai kuwa amekuwa akiiomba manispaa kulijenga soko hilo lakini amekuwa akipewa ahadi zisizotekelezeka.

Comments are closed.