WAFANYABIASHARA TEGETA KWA NDEFU WAIOMBA SERIKALI KUWATENGEA ENEO MAALUM LA SOKO

WAFANYABIASHARA TEGETA KWA NDEFU WAIOMBA SERIKALI KUWATENGEA ENEO MAALUM LA SOKO

Like
327
0
Wednesday, 13 January 2016
Local News

WAFANYABIASHARA  wa soko lisilo rasmi lililopo tegeta kwa ndevu  Jijini  Dar es salaam wameiomba serikali kuwatengea eneo maalum la kufanyia biashara zao kutokana soko la nyuki  lililotengwa  kuwa finyu  hali inayosababisha wao kuendelea kuwepo sokoni hapo.

 

Wakizungumza na efm Jijini  Dar es salaam Wafanya Biashara hao wamesema kuwa  kipinndi cha nyuma eneo hilo lilikuwa lipo chini ya serikali  ya mtaa ambapo kwa sasa linamilikiwa na mtu binafsi ambae ndie amewapangisha.

 

Kwa upande wake, Mwenyekiti  wa Soko hilo RAMADHAN  HUSSEN amesema kuwa eneo la nyuki liliotengwa kwaajili ya wafanya biashara hao ni eneo la boko na siyo Tegeta ambapo pia ameshawahi kuongea na serikali ya mtaa huo kuhusu eneo hilo kulifanya liwe rasmi kwaajili ya wafanyabiashara kufanya biashara zao lakini mpaka sasa suala hilo halijafanikiwa.

Comments are closed.