WAFANYABIASHARA WAIOMBA TRA KUWA NA MFUMO WA WAZI WA MASHINE ZA EFD

WAFANYABIASHARA WAIOMBA TRA KUWA NA MFUMO WA WAZI WA MASHINE ZA EFD

Like
263
0
Tuesday, 16 December 2014
Local News

WAFANYABIASHARA nchini wameiomba mamlaka ya mapato Tanzania TRA kutengeneza utaratibu utakaoonyesha stakabadhi za Manunuzi,uendeshaji na uuzaji wa bidhaa katika mashine za kierectroniki za EFD.

Akiongea na EFM kwa niaba ya wafanyabiashara leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa taifa wa jumuiya wafanyabiashara JOHNSON MINJA amesema wafanyabiashara hawagomi kutumia mashine za EFD kama inavyosemwa na baadhi ya watu ila wanachohitaji ni kuwepo kwa mifumo hiyo mitatu ya wazi itakayoonyesha kila kitu.

Minja amesema uwepo wa utoaji wa stakabadhi tatu utasaidia wafanyabiashara kulipa kodi kwa uaminifu kwani anapokuwa anafahamu mzigo wake alionunua ataulipia kodi kiasi gani,pamoja na ongezeko la kodi kutoka kwa wafanyabiashara hao pia itasaidia kupunguza msongamano katika bandari.

Aidha alisema ni wakati sasa serikali iangalie utaratibu wa kuacha kufuata mifumo inayowadidimiza wafanyabiashara na badala yake itoe utaratibu wa wazi utakaooonyesha namna mfanyabiashara anavyotakiwa kulipa kodi zake kwa uhalali kupitia mashine hizo za EFD.

Comments are closed.