WAFANYAKAZI KATIKA KISIMA CHA MAFUTA WAUAWA LIBYA

WAFANYAKAZI KATIKA KISIMA CHA MAFUTA WAUAWA LIBYA

Like
464
0
Thursday, 05 February 2015
Global News

HABARI kutoka Libya zinasema kuwa idadi kadha ya wafanyakazi katika kisima kimoja cha mafuta wameuawa katika shambulio moja Jumanne usiku.

Afisa mmoja mwandamizi wa kijeshi amesema kuwa watu kumi na watatu wameuawa katika kisima cha Mabrook. Watano ni raia wa kigeni, watatu wakiwa ni Wafilipino na wawili wanatoka Ghana.

Afisa huyo amesema kuwa wote waliouawa walikatwa koromeo, mbali na Mlibya mmoja ambaye alipigwa risasi. Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, ingawa taarifa za watu walioshuhudia tukio hilo wanasema watu wenye silaha wakijitangaza kuwa wanachama wa kundi la Islamic State ndio waliohusika na mauaji hayo.

Comments are closed.