WAFANYAKAZI MUHIMBILI WAMETAKIWA KUWAHI NA KUFANYA KAZI KWA BIDII

WAFANYAKAZI MUHIMBILI WAMETAKIWA KUWAHI NA KUFANYA KAZI KWA BIDII

Like
267
0
Wednesday, 11 November 2015
Local News

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru ameanza kazi rasmi na kuwataka wafanyakazi wa hospitali hiyo kuwahi kazini kwa wakati na kufanya kazi kwa bidii.

 

Profesa Mseru ametoa kauli hiyo jana Jijini Dar es salaam baada ya kukutana na menejimenti ya hospitali hiyo ambayo inajumuisha Wakurugenzi 14.

 

Profesa Mseru ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo baada ya dokta Hussein Kidanto kuhamishiwa wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.

Comments are closed.