ZAIDI ya wafanyakazi 800 wa kampuni ya ujenzi ya chiko ya Jamuhuri ya china inayojenga barabara kuu ya Dodoma Babati eneo la mayamaya mpaka mela wamegoma wakishinikiza uongozi wa kampuni hiyo uboreshe maslahi yao kwa kuwapatia mikataba pamoja na kuongeza mishahara huku wakitaka serikali kuwafukuza wafanyakazi wa kigeni ambao wanapora ajira zinazoweza kufanywa na wazawa huku wakilipwa mamilioni ya fedha.
Wakizungumza mbele ya waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano profesa Makame mbarawa wafanyakazi hao wamesema wamechoshwa na vitendo vya unyanyasaji wanavyo fanyiwa na wakandarasi kutoka uchina huku wakilipwa mishahara duni na kila wanaposhinikiza madai yao wanapuuzwa.