WAFUGAJI KUONDOKANA NA VIFO VYA MIFUGO

WAFUGAJI KUONDOKANA NA VIFO VYA MIFUGO

Like
234
0
Tuesday, 20 October 2015
Local News

WAFUGAJI nchini wanatarajia kuondokana na hasara ya vifo vya mifugo yao ikiwemo ng’ombe, baada ya kuzinduliwa dawa mpya ijulikanayo kwa jina la Vectoclor Plus, inayodhibiti magonjwa yanayoenezwa na  Kupe.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa
Kitengo cha Udhibiti wa wadudu na magonjwa yaenezayo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dokta Martin Ruheta, amesema uzinduzi huo umekuja wakati muafaka, kwani utapunguza vifo vya mifugo ambapo kila mwaka wanyama wanakufa kwa asilimia 70 kwa sababu ya magonjwa ya mbung’o na Kupe.
Dokta Ruheta amesema kwamba dawa hiyo imechanganywa na dawa nne na zenye nguvu ya kuua wadudu hao kwa kiwango kikubwa na Inzi wanaofuata wanyama.

Comments are closed.