WAFUGAJI WAMETAKIWA KUUZA MIFUGO KUNUNUA VYAKULA SIMANJIRO

WAFUGAJI WAMETAKIWA KUUZA MIFUGO KUNUNUA VYAKULA SIMANJIRO

Like
330
0
Wednesday, 04 November 2015
Local News

MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewataka wafugaji wa wilaya hiyo kupunguza mifugo yao kwa kuiuza ili wanunue vyakula kwenye wakati huu unaokabiliwa na upungufu wa chakula.

 

Kambona ameyasema hayo wakati akizungumzia tukio la Tarafa ya Moipo kupatiwa msaada wa chakula tani 150 za mahindi zilizotolewa na serikali kutokana na eneo hilo kukumbwa na ukame hivyo kukosa chakula. Amesema tani hizo 150 za mahindi baadhi yake zitauzwa sh500 kwa kila kilo moja na sh5,000 kwa gunia lenye uzani wa kilo 100 na jamii yenye uhitaji maalumu wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu, watapatiwa mahindi hayo bure.

 

Comments are closed.