WAFUNGWA WATOROKA GEREZANI AFRIKA YA KATI

WAFUNGWA WATOROKA GEREZANI AFRIKA YA KATI

Like
285
0
Tuesday, 29 September 2015
Global News

MAMIA ya wafungwa katika Gereza moja nchini jamuhuri ya Afrika ya kati wametoroka wakati ambapo kumekuwa na machafuko yaliyosababisha baadhi ya watu kupoteza maisha.

Hali hiyo imekuja baada ya dereva wa gari ndogo muumini wa dini ya kiislamu kuuawa na kusababisha kuibuka kwa mapigano siku ya jumamosi kati ya wanamgambo wa kikristo na makundi ya kiislamu.

Wafuasi wa wanamgambo wa kikristo wajulikanao kwa jina Anti-Balaka walishambulia gereza siku ya jumatatu na kuwatorosha mamia ya Wanajeshi na wanamgambo.

Comments are closed.