WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee imewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasimamie utekelezaji wa mikakati yote ya kudhibiti mlipuko wa kipindupindu ikiwa ni pamoja na kusimamia kanuni za afya na kuhakikisha kuwa wanadhibiti ugonjwa huo kwa kutoa taarifa ya utekelezaji kila siku .
Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam Waziri wa Wizara hiyo Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema licha ya kasi ya ongezeko la ugonjwa huo kupungua Dar es salaam kutoka wastani wa wagonjwa 80 kwa mwezi Septemba kufikia wastani wa wagonjwa 6 kwa mwezi huu wa Disemba, kumeripotiwa kuwepo kwa wagonjwa 6 wapya katika Manispaa ya Ilala hivyo Wananchi waendelee kuzingatia kanuni za afya za usafi kwa kuwa ugonjwa huo bado upo.