WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAMETAKIWA KUSIMAMIA MIKAKATI YA KUDHIBITI KIPINDUPINDU

WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAMETAKIWA KUSIMAMIA MIKAKATI YA KUDHIBITI KIPINDUPINDU

Like
210
0
Wednesday, 16 December 2015
Local News

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto  na Wazee imewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wasimamie utekelezaji wa mikakati yote ya kudhibiti mlipuko wa kipindupindu ikiwa  ni pamoja na kusimamia kanuni za afya na kuhakikisha kuwa wanadhibiti ugonjwa huo  kwa kutoa taarifa ya utekelezaji kila siku .

 

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam  Waziri wa Wizara hiyo  Mheshimiwa  Ummy Mwalimu amesema licha ya kasi ya ongezeko la ugonjwa huo kupungua Dar es salaam kutoka wastani wa wagonjwa 80 kwa mwezi Septemba kufikia wastani wa wagonjwa 6 kwa mwezi huu wa Disemba,  kumeripotiwa kuwepo kwa wagonjwa 6 wapya katika Manispaa ya Ilala hivyo Wananchi waendelee kuzingatia kanuni za afya za usafi kwa kuwa ugonjwa huo bado upo.

 

Comments are closed.