WAGOMBEA URAIS KUPITIA CCK NA ADC WANATARAJIWA KUCHUKUA FOMU NEC LEO

WAGOMBEA URAIS KUPITIA CCK NA ADC WANATARAJIWA KUCHUKUA FOMU NEC LEO

Like
210
0
Friday, 07 August 2015
Local News

WAGOMBEA urais kupitia chama cha Kijamii-CCK na Alliance for Democratic Change-ADC, leo wanatarajiwa kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC , Jijini Dar es salaam.

Hivi karibuni ADC ilimtangaza Chifu Lutalosa Yemba kuwa mgombea wake wa urais huku Mwenyekiti wa chama hicho Said Miraji Abdallah akitajwa kuwa mgombea mwenzake.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi-NEC, baada ya vyama hivyo viwili kuchukua fomu leo, itafuatiwa na na ACT Wazalendo ambapo mgombea wake anatarajiwa kuchukua fomu Agost 10 mwaka huu siku mbili baada ya kutangazwa na chama hicho.

Comments are closed.