WAGOMBEA WA NAFASI ZA URAIS WAREJESHA FOMU LEO

WAGOMBEA WA NAFASI ZA URAIS WAREJESHA FOMU LEO

Like
245
0
Friday, 21 August 2015
Local News

WAGOMBEA mbalimbali wa nafasi za urais leo wamerejesha fomu zao katika Tume ya Uchaguzi- NEC, tayari kwa uzinduzi wa Kampeni kuelekea uchaguzi Mkuu oktoba 25 mwaka huu.

 

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu yake, mgombea kupitia chama cha  mapinduzi- CCM Dokta John Magufuli amesema ametimiza matakwa yote ya kisheria na sasa kilichobaki ni uzinduzi wa kampeni.

 

Kwa upande wake mgombea wa nafasi ya urais kupitia vyama vinavyounda umoja wa katiba UKAWA Edward Lowasa,

amewataka viongozi na wanachama kumuunga mkono katika safari yake ya matumaini kuelekea Ikulu.

 

Comments are closed.