WAHAMIAJI HARAMU: KAULI YA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA YAZUA UTATA

WAHAMIAJI HARAMU: KAULI YA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA YAZUA UTATA

Like
244
0
Thursday, 30 July 2015
Global News

WAZIRI Mkuu wa Uingereza ameibua utata kwa kutoa maneno ya kuwafananisha wahamiaji haramu wanaojaribu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza kuwa wao ni kama kundi la nyuki.

Baraza linalowashughulikia wakimbizi Nchini Uingereza limesema kuwa hiyo haioneshi thamani kwa watu na ni hatari zaidi kwa kuwa imetoka kinywani mwa kiongozi mwenye hadhi kubwa duniani.

Waziri huyo mkuu ambaye yuko ziarani Vietnam alikuwa akitoa maoni kuhusiana na vurugu zinazoendelea katika mji wa Calais nchini Ufaransa ambapo mamia ya wahamiaji wamekimbia kuelekea Uingereza.

 

Comments are closed.