WAHAMIAJI wengi zaidi wanaendelea kuwasili nchini Bulgaria licha ya kuongeza ulinzi katika mipaka yake, kuweka kamera na vifaa vitakavyotambua nyendo za watu na kurefusha uzio wa usalama wenye urefu wa kilometa 160 ambao umejengwa kwenye mpaka wake na Uturuki.
Data rasmi zinaonyesha kuwa kiasi cha watu elfu 25,000 wamejiandikisha kama wakimbizi nchini Bulgaria katika miaka miwili iliyopita, hiyo ikiwa ni idadi na ile iliyoandikishwa katika muda wa miongo miwili iliyopita.
Wakimbizi kutoka Syria au Afghanistan , wengi wanakimbia mizozo katika nchi zao pamoja na umasikini na wanamatumaini ya kuitumia nchi hiyo kama njia ya kupata maisha bora zaidi katika bara la Ulaya.