WAHAMIAJI WAZIDI KUWASILI BULGARIA

WAHAMIAJI WAZIDI KUWASILI BULGARIA

Like
149
0
Thursday, 20 August 2015
Global News

WAHAMIAJI  wengi  zaidi wanaendelea  kuwasili   nchini Bulgaria licha  ya  kuongeza  ulinzi  katika  mipaka  yake, kuweka  kamera na  vifaa  vitakavyotambua  nyendo  za watu na  kurefusha  uzio  wa  usalama  wenye urefu wa kilometa 160 ambao  umejengwa kwenye mpaka  wake  na Uturuki.

Data rasmi zinaonyesha kuwa kiasi  cha watu elfu 25,000 wamejiandikisha  kama  wakimbizi nchini  Bulgaria  katika miaka  miwili  iliyopita, hiyo ikiwa  ni  idadi na ile iliyoandikishwa katika  muda wa miongo  miwili  iliyopita.

Wakimbizi  kutoka  Syria  au Afghanistan , wengi wanakimbia mizozo  katika  nchi  zao  pamoja  na umasikini  na  wanamatumaini  ya  kuitumia  nchi  hiyo kama  njia  ya  kupata maisha  bora  zaidi  katika  bara  la Ulaya.

 

Comments are closed.